DIAMOND, AUNT WAONGOZA SHANGWE ‘BIRTHDAY’ YA MOSE IYOBO

DIAMOND, AUNT WAONGOZA SHANGWE ‘BIRTHDAY’ YA MOSE IYOBO



USIKU wa kuamkia leo dansa wa Crow ya Wasafi Classic Baby, Mose Iyobo, alisherehekea siku ya kuzaliwa kwake iliyohudhuriwa na  baadhi ya mastaa akiwemo bosi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’, na mzazi mwenzake, Aunt Ezekiel, ambapo kwa pamoja waliongoza shangwe kwenye pati hiyo.
Hafla hiyo ilifanyika ndani ya ukumbi wa hoteli ya Regence iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam, ambapo mastaa na watu kibao  walihudhuria wakanywa na kukata keki iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa sherehe hizo.