(Video) Collabo ya Ally Kiba na Fally Ipupa iko tayari! Ally Kiba athibitisha hilo.

(Video) Collabo ya Ally Kiba na Fally Ipupa iko tayari! Ally Kiba athibitisha hilo.


Video Interview

Mwana ilikuwa ni nyimbo ambayo nifanye na Fally Ipupa, beat imetengenezwa na Man Walter. Lakini kitu ambacho kilikwenda kutokea wakati nakwenda studio kufanya nyimbo nyingine kabisa, nikakuta Man Walter ameniandalia beat, ‘ile nyimbo yako unataka kufanya na Fally Ipupa hii hapa.’ Akaweka beat nikaanza ku-flow pale, nikaimbaimba nikapata melody. Kesho yake nikarudi nikafanya demo, kufanya demo nikarudi nyumbani nikakaa kama wiki, baada ya wiki moja nikaenda nikaimaliza yote, Lakini sasa tukakaa na Man Walter nikasema Fally Ipupa anaimbaje hapa? Akasema kwa kweli umeperfome vizuri sana, mimi naona ume-perfome vizuri sana. Tukapanga tufanye nyimbo nyingine. Basi akasema poa lakini Mwana ilikuwa Fally Ipupa aimbe. Kolabo na Fally Ipupa ipo, lakini kama ilivyo kawaida yangu napendaga kuwa-surprise watu kwa sababu watu wanakuwa hawajui Ali anafanya kitu gani muda wowote. Lakini ngoma ya Fally na mimi ipo na siwezi sema ni nyimbo gani lakini nyimbo ni nzuri sana na imesharekodiwa“.